JINSI YA KUONGEZA KUJIAMINI KATIKA MAISHA YAKO

HABARI ZENU WAPENDWA WANGU, KARIBUNI TENA KATIKA KURASA ZETU TUNAZOWEZA KUJIFUNZA NA KUONGEZA UJUZI WA MAMBO MBALIMBALI KUHUSU UREMBO, SANAA NA HATA KUPATA MAFUNDISHO YATAYOKUSAIDIA KATIKA MAISHA YAKO YA KILA SIKU.

NI JAMBO LISILOPINGIKA KUWA KATIKA MAISHA KILA MTU ANATAMANI KUJIAMINI, PAMOJA YA KUWA KUNA MAMBO MENGI YANAYOWEZA KUKUFANYA UWEZE KUJIAMINI KATIKA MAISHA YAKO, TUSISAHAU KWA WANAWAKE UREMBO NI MOJA KATI YA NGUZO KUU KATIKA HILI.

LEO TUTAENDA KUTAZAMA MAMBO KADHAA YATAYOKUONGEZEA KUJIAMINI, 



KUJIAMINI #Confidence..
Ama kwa hakika kila mtu anapenda kujiamini, kila mtu anatamani afanye jambo pasi kuwepo na hofu ndani ya moyo wake, hofu itakayomzuia ashindwe kuwa na nguvu ya kufanya, kuamua ama kuzungumza chochote kulingana na hisia zake..
Leo nitakupatia mambo matatu 3 yatayokuongezea kujiamini.

1. LAZIME UTAMBUE NINI NINAKUFANYA USIJIAMINI/
Hii inaweza kuwa muonekano wako, inaweza kuwa hali yako ya kiuchumi lakini pia inaweza kusababishwa na mazingira ama watu wanaokuzunguka, Kulijua tatizo ni nusu ya kuwa umeshalitatua, jaribu kuanza taratibu kubadilisha hicho utachogundua kinakufanya ukose #confidence, hatua hii itachukua muda kidogo lakini hakika mara baada ya kuimaliza utakuwa umepiga hatua kubwa katika kuongeza kujiamini kwako...

2. ACHA KUJILINGANISHA NA WATU WENGINE
Kujilinganisha na mtu fulani aliyekuzidi hali fulani ya uwezo kunapelekea kuathiri kujiamini kwako moja kwa moja, hivyo lazima ukubali kuwa wewe ni nani na yeye ni nani, ujipe thamani mara 2 ya utakavyompa mtu ambaye unamtazama mbele yako, ni lazima utambue kuwa kuna watu wamekuzidi wewe uwezo ila pia wapo watu ambao umewazidi wewe uwezo.

3. JIPENDE, JITUNZE, JITHAMINI
Jipatie vitu ambavyo unapenda kuvifanya, yaani kama unapenda kuvaa vizuri kupendeza, unapenda kutoka out na marafiki zako, hii itarudisha furaha na uchangamfu ndani yako kitu ambacho moja kwa moja kitapelekea kukufanya ujiamini zaidi, ukija kufuatilia utagundua kuwa asilimia 65 ya watu ambao wanakosa kujiamini ni wale ambao hawana furaha, pigania furaha yako.
Ukizingatia mambo haya matatu hakika utarudisha hali ya kujiamini katika maisha
Kwa maoni,
0766 641 185
Facebook @ Faith Msuya
Instagram @ FaithMsuya
Email | iamfaithmsuya@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

TAFSIRI YA UREMBO

JIFUNZE KUCHEZA NA RANGI YA VIPODOZI KATIKA KUKAMILISHA UREMBO WAKO