TAFSIRI YA UREMBO
Urembo siku hizi ni mtaji au daraja la kupata mambo mengi maishani. Ukishabikia sana kujenga tabia njema ukasahau kuboresha urembo basi unaweza kupitwa na fursa mbalimbali ikiwemo uchumba na ndoa. Sijawahi kusikia mwanaume akifanya “ waxing ya ndevu” aumie kwa ajili ya kuwa soft ili ndevu zisimkwaruze mwanamke…! Amkeni! Misemo imesheheni siku hizi utasikia “Mwanamke urembo”! Hivi uzuri au urembo wa mwanamke wa kiafrika siku hizi ni nini? Wahenga walikuwa na usemi “Uzuri wa mwanamke siyo sura au urembo bali ni tabia njema”. Methali hii sina hakika kama bado inabeba maana yoyote kwa sababu kila mwanamke anahangaikia sana urembo na katika mahangaiko hayo huweza kujikuta akisahau kutunza tabia njema. Kwanini hali imekuwa hivyo, ni swali la kujiuliza. Urembo siku hizi ni mtaji au daraja la kupata mambo mengi maishani. Ukishabikia sana kujenga tabia njema ukasahau kuboresha urembo basi unaweza kupitwa na fursa mbalimbali ikiwemo uchumba na ndoa. Hata hivyo kwa miaka ya siku ...